Radio Kwizera
Radio Kwizera
April 20, 2026, 7:01 pm

Mradi huo utagharimu shilingi milioni 10 ikiwa ni sehemu ya mikakati ya kuongeza kipato chao ndani ya kanisa ambapo mradi umefikia hatua ya msingi.
Na Samwel Masunzu- Kakonko, KIGOMA
Wanawake katika kanisa la Free Pentecostal Church FPCT Kakonko mjini mkoani Kigoma wameanzisha mradi wa nyumba ya kupangisha utakaowawezesha kuongeza kipato
Akisoma risla ya umoja wa wanawake hao UWW, Katibu wa wanawake wa Kanisa hilo Mercy Prosper amesema mradi huo utagharimu shilingi milioni 10 ikiwa ni sehemu ya mikakati ya kuongeza kipato chao ndani ya kanisa ambapo mradi umefikia hatua ya msingi.
Redio Kwizera imezungumza na Mwenyekiti wa UWW, Evelyn Erasto ambaye amesema mradi wa nyumba hiyo utawawezesha kupata shilingi laki 2 kila mwezi
Mgeni rasmi katika sherehe hiyo ya wanawake Afisa Elimu Idara ya Msingi Kakonko Bi. Isabella Mwakabonga akiendesha harambee ya kuchagia ujenzi huo, amewataka wanawake hao kutokujihusisha na migogoro wakati wa usimamizi wa mradi huo kabla na baada ya kukamilika.
Sikukuu ya wanawake katika Kanisa hilo imetanguliwa na shughuli mbalimbali tangu April 16 na kutamatika Aprili 19 ambapo usimamizi wa ibada na huduma nyingine umefanyika chini ya wanawake.
Naye mchungaji wa kanisa hilo Mathias Ndabunganiye amewapongeza wanawake kwa jitihada zao za kufanikisha shughuli hiyo pamoja na wale ambao wameweza kuwaunga mkono