Radio Kwizera

Taa za barabarani zaing’arisha Kibondo, Kigoma

May 2, 2026, 3:22 pm

Mwonekano wa Usiku baada ya baadhi ya Barabara mjini Kibondo kuwekewa taa. Picha na Samwel Masunzu

Mkakati uliopo ni kuhakikisha mji wa Kibondo unakuwa na taa za kutosha zitakazoruhusu shughuli nyingine kufanyika hata majira ya usiku.

Na Samwel Masunzu- Kibondo, KIGOMA

Halmashauri ya wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma kupitia wakala wa barabara za mijini na vijijini TARURA imesema kwa sasa barabara zote za mjini zinazojengwa kwa kiwango cha lami zitawekwa taa za barabarani ili kupendezesha mji huo hasa nyakati za usiku.

Meneja wa TARURA wilaya ya Kibondo Mhandisi Dickson Kanyankole amesema mkakati huo ni kuhakikisha mji wa Kibondo unakuwa na taa za kutosha zitakazoruhusu shughuli nyingine kufanyika hata majira ya usiku

Baadhi ya wakazi mjini Kibondo wamesema uwepo wa taa za barabani umesaidia pia kupunguza uhalifu kutokana na mwanga uliopo sambamba na kuwasaidia kufanya biashara ndogondogo kando ya barabara.