Radio Kwizera
Radio Kwizera
April 28, 2026, 3:21 pm

Amina ameahidi kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kuitendea haki tuzo hiyo, huku akisisitiza dhamira yake ya kuiwakilisha vyema sekta ya habari pamoja na wanawake na wanaume wa Kanda ya Ziwa na Tanzania kwa ujumla.
MWANZA
Mwandishi wa habari wa Radio Kwizera FM Amina Semagogwa, ameibuka mshindi wa tuzo ya Mwanamke Kinara Kanda ya Ziwa katika Sekta ya Habari kwa mwaka 2026.
Mara baada ya ushindi huo, Amina amesema mafanikio hayo yametokana kwa kiasi kikubwa na kura za wananchi, ambapo amesema asilimia 40 ya kura hizo zimechangia kumfikisha hatua hiyo muhimu katika taaluma yake.
Ameeleza kuwa kila kura aliyopata imebeba upendo, imani na matumaini kutoka kwa waliomuunga mkono, na kutoa shukrani za dhati kwa wote waliomchagua na kusimama naye katika safari hiyo.
Aidha, Amina ameahidi kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kuitendea haki tuzo hiyo, huku akisisitiza dhamira yake ya kuiwakilisha vyema sekta ya habari pamoja na wanawake na wanaume wa Kanda ya Ziwa na Tanzania kwa ujumla.
Amehitimisha kwa kuwashukuru wadau wote na kusisitiza kuwa ushindi huo ni chachu ya kuongeza juhudi katika kazi yake ya uandishi wa habari.
Kwa niaba ya Uongozi wa Radio Kwizera tunakupongeza sana Amina