Radio Kwizera

Mitazamo hasi kuhusu Malaria yakemewa Muleba

April 28, 2026, 1:06 pm

Wakazi wa Wilaya ya Muleba waliohudhuria Maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani ambayo ki Wilaya yamefanyika April 25, 2026 Kata ya Kyebitembe kijiji cha Kasindaga.

Wananchi wamehimizwa kuzingatia ushauri wa wataalamu wa afya, kutumia vyandarua vyenye viuatilifu pamoja na kudumisha usafi wa mazingira ili kupunguza mazalia ya mbu.

Na Shafiru Yusuph- Muleba, KAGERA

Wakazi wa Wilaya ya Muleba Mkoani Kagera wametakiwa kuondoa mitazamo hasi pindi wanapopata dalili za ugonjwa wa malaria na badala yake kufika mapema kwenye vituo vya afya kwa ajili ya uchunguzi na matibabu sahihi.

Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Muleba Bw. Evart Kagaruki ambaye amemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Muleba amesema hayo kwenye maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani ambayo ki Wilaya yamefanyika Kata ya Kyebitembe kijiji cha Kasindaga.

Bw. Kagaruki amesema kuwa kuchelewa kutafuta matibabu kunachangia kuongezeka kwa madhara ya ugonjwa huo ikiwa ni pamoja na vifo vinavyoweza kuzuilika.

Aidha, wananchi wamehimizwa kuzingatia ushauri wa wataalamu wa afya, kutumia vyandarua vyenye viuatilifu pamoja na kudumisha usafi wa mazingira ili kupunguza mazalia ya mbu.