Radio Kwizera
Radio Kwizera
May 2, 2026, 3:05 pm

Bonanza hilo lengo lake ni kuhamasisha jamii kupinga ukatili, kuhamasisha malezi bora kwa watoto, kuwa karibu na polisi, kusomesha watoto, kutii sheria, kupinga imani potofu, kukataa uhamiaji haramu na kutoa taarifa za uhalifu.
Na Samwel Masunzu- Kibondo, KIGOMA
Watumishi wa Umma kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi na jamii katika kata ya Nyaruyoba wilayani Kibondo mkoani Kigoma wameungana pamoja kuadhimisha sikukuu ya wafanyakazi (Mei Mosi)
Maadhimisho hayo yamefanyika kwenye uwanja wa shule ya msingi Nyaruyoba ‘B’ ambapo elimu ya kupinga ukatili, rushwa na uhalifu imetolewa kupitia bonanza la michezo.
Polisi Kata,wa kata ya Nyaruyoba Insp. Singila Magesa amesema bonanza hilo lengo lake ni kuhamasisha jamii kupinga ukatili, kuhamasisha malezi bora kwa watoto, kuwa karibu na polisi, kusomesha watoto, kutii sheria, kupinga imani potofu, kukataa uhamiaji haramu na kutoa taarifa za uhalifu.
Naye Mkuu wa Polisi Jamii wilaya ya Kibondo ASP Makwasa Makwasa amepongeza Polisi Kata na watumishi kwa kuanda bonanza hilo, na kwamba hali hiyo inaonyesha mshikamano ulipo kati ya Jeshi la Polisi, watumishi pamoja na jamii
Katika bonanza hilo watumishi na wananchi wengine wameshiriki michezo ya pamoja ikiwemo kuvuta kamba, kukimbia na yai kwenye kijiko, kukimbia kweye gunia, kukimbiza kuku pamoja na mpira wa miguu kati ya watumishi na timu ya Hunters.
Bonanza hilo limeongozwa na Kaulimbiu isemayo “Polisi na Jamii kwa pamoja tunaweza kutokomeza uhalifu”