Radio Kwizera

Ushirikiano na jamii ni msingi wa kiroho- Mch. Luhumbi

November 4, 2026, 6:37 pm

Baadhi ya Waumini wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God TAG Yordani mji mwema Kibondo wakiwa katika ibada ya kuzindua kanisa hilo. Picha na Samwel Masunzu

Ushirikiano na jamii ni suala ambalo litajenga uimara wa utoaji wa huduma za kiroho katika jamii badala ya kujitenga

Na Samwel Masunzu- Kibondo, Kigoma.

Makamu Askofu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God TAG Jimbo la Kigoma Kaskazini Mch. Robert Luhumbi amewataka viongozi wa makanisa kuendelea kushirikiana na jamii katika huduma mbalimbali

Mchungaji Luhumbi ameeleza hayo wakati akizindua Kanisa la TAG Yordani mji mwema Kibondo mkoani Kigoma na kwamba ushirikiano na jamii ni suala ambalo litajenga uimara wa utoaji wa huduma za kiroho katika jamii badala ya kujitenga

Mchungaji wa Kanisa la TAG Yordani ambaye amesimikwa na kuwekwa wakfu, Elia Ntambala amelishukuru kanisa mama la AGAPE na kuahidi kuendelea kutoa huduma kwa mjibu wa taratibu za kanisa hilo.

Baadhi ya wazee wa kanisa wa kanisa la TAG AGAPE, Bw. Emmanuel Solomon na Bi. Kevina Lugakingira wamesema ujenzi wa kanisa hilo umetokana na jitihada za kamati ya ujenzi kwa kushirikiana na waumini kwa lengo la kuendelea kuhubiri habari njema.

Kanisa la TAG AGAPE limefikisha idadi ya makanisa 5 ambayo yemejengwa na kuweka wachungaji ambao wanahitimu masomo ya biblia na kuanza huduma ya utumishi