Radio Kwizera
Radio Kwizera
October 9, 2026, 12:36 pm

Wazee wametakiwa kutambua kuwa kujichukulia sheria mkononi kunaweza kusababisha uvunjifu wa amani, migogoro katika jamii na hata kuwafanya wahusika kukabiliwa na hatua za kisheria.
Na Shafiru Yusuph- Muleba, Kagera
Wazee wilayani Muleba, mkoani Kagera, wametakiwa kuepuka kujichukulia sheria mkononi kutokana na kukata tamaa za maisha, badala yake wametakiwa kutumia njia za kisheria kutatua changamoto zinazowakabili.
Wito huo umetolewa na Afisa Tarafa ya Nshamba Bi. Kelementina Msafiri wakati alipomwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Muleba Dkt. Abel Nyamahanga kwenye Maadhimisho ya siku ya Wazee Duniani ambayo imeadhimishwa leo kata ya Nshamba.
Bi. Msafiri amesema wazee wametakiwa kutambua kuwa kujichukulia sheria mkononi kunaweza kusababisha uvunjifu wa amani, migogoro katika jamii na hata kuwafanya wahusika kukabiliwa na hatua za kisheria.
Baadhi ya wazee wamesema kuna haja ya Serikali kuendelea kuwajali na kuwasaidia wazee, hususan wale wanaokabiliwa na changamoto za kiuchumi na kijamii, ili kupunguza hali ya kukata tamaa na kuwawezesha kuishi kwa amani na usalama.
