Radio Kwizera

DC Kibondo asisitiza ulinzi na usalama

October 9, 2026, 1:54 pm

SACP Selemani Enock Nyakulinga (kushoto) na Mkuu wa wilaya mstaafu Kanali mstaafu Aggrey Magwaza wakisaini wakati wa makabidhiano ya ofisi. Picha na Samwel Masunzu

SACP Nyakulinga ameitaka kamati ya ulinzi na usalama kuendelea kuimarisha ulinzi na usalama

Na Samwel Masunzu- Kibondo, KIGOMA.

Mkuu mpya wa wilaya ya Kibondo Kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi SACP Selemani Enock Nyakulinga amekabidhiwa rasmi ofisi na kuanzia majukumu ya kuwatumikiwa wananchi wa wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma.

Katika hafla ya makabidhiano ambao imefanyika ofisi ya mkuu wa wilaya, SACP Nyakulinga ameitaka kamati ya ulinzi na usalama kuendelea kuimarisha ulinzi na usalama ili wananachi wafanye shughuli zao kwa amani.

Aidha amesisitiza kila mmoja kuwajibika katika nafasi yake na kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua.

Mkuu wa wilaya mstaafu Kanali mstaafu Aggrey Magwaza amewashukuru watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Kibondo pamoja na wananchi kwa kushirikiana katika kutimiza malengo ya serikali huku akisisitiza kuendelea kuwepo kwa ushirikiano.

Baadhi ya washiriki katika hafla hiyo wakiwemo wawakilishi wa vyama vya siasa, uongozi wa wafanyabiashara, na viongozi wa dini wamemkaribisha mkuu wa wilaya mpya na kumuahidi ushirikiano na kumtakia kila heri mkuu wa wilaya mstaafu Kanali Magwaza