Radio Kwizera

Zaidi ya abiria 40 wanusurika kifo baada ya basi kuungua, Kahama

November 13, 2026, 11:41 am

Baadhi ya Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakiwa eneo la tukio ambapo Basi la Abood limeteketea kwa moto. Picha na Mtandao

Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Wilaya ya Kahama, SSP Stanley Luhwago, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo

Na Marco Pastory.

Zaidi ya abiria 40 wamenusurika katika tukio la moto lililoteketeza basi la Kampuni ya Usafirishaji ya Abood katika eneo la Isaka, Wilaya ya Kahama, Mkoa wa Shinyanga.

Basi hilo lenye namba za usajili T 285 EAV lilikuwa likitoka Dar es Salaam kuelekea Kagera, kabla ya kukumbwa na tukio hilo leo Novemba 13, 2026, majira ya saa 11 alfajiri.

Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Wilaya ya Kahama, SSP Stanley Luhwago, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kikosi cha zimamoto kilifanikiwa kuufikia eneo la tukio na kuuzima moto huo.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa, hakuna abiria aliyeripotiwa kupoteza maisha, ingawa basi hilo limeteketea kwa moto huku chanzo cha kutokea kwa moto huo zikiwa bado hazijajulikana.