Radio Kwizera

Mvua ya upepo yaacha nyumba 9 bila makazi, Biharamulo

November 13, 2026, 7:07 pm

Baadhi ya Waathirika wa mvua ya Upepo Nyantakara, Biharamulo wakiwa na Viongozi wa Halmashauri baada ya kupatiwa msaada wa vitu mbalimbali. Picha na William Mpanju

Kamati ya maafa ya halmashauri ya Wilaya Biharamulo wametoa msaada wa vyakula ikiwemo unga kg 5 kila mmoja pamoja na maharage na maji ya kunywa.

Na William Mpanju-Biharamulo, KAGERA.

Kamati ya maafa ya halmashauri ya Wilaya Biharamulo mkoani Kagera imetembelea waathirika wa tukio la mvua kubwa iliyoambana na upepo kuezua nyumba 9 za wakazi wa Kijiji Cha Kasiro Kata ya Nyantakara wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera.

Kamati hiyo iliyoongozwa na Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya Biharamulo Bw. Innocent Mukandala ambapo wametoa msaada wa vyakula ikiwemo unga kg 5 kila mmoja pamoja na maharage na maji ya kunywa.

Mukandala amesema wananchi wanapaswa kuendelea kuchukua tahadhali kwani bado mvua zinaendelea kunyesha hivyo ni muhimu kuzingatia maelekezo yaliyotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) iliyotoa tahadhari ya mvua za El Nino.

Mratibu wa maafa wilaya ya Biharamulo Bw. Abdalah Ndushi amesema tukio hilo limetokea Nov 6, 2026 mwaka huu majira ya saa 8 mchana ambapo waathirika wa mvua hiyo ni 9 na baadhi ya mashamba ya mazao kuharibika.

Mtendaji wa Kata ya Nyantakara Bw. Omary Sempory amesema wanaendelea kutoa elimu kwa wananchi wa Kata hiyo ili kuepuka madhara mengine kama hayo ya mvua za El nino nakwamba miongoni mwa waathirika ni Mzee wa miaka 70