Radio Kwizera

DW Akademie yawanoa wanahabari matumizi ya AI

October 9, 2026, 1:42 pm

Waandishi wa habari, Watangazaji na Wataalamu wa Teknolojia waliohudhuria mafunzo ya DW Akademie juu ya matumizi sahihi ya AI. Picha na David Mwaluseke.

Lengo ni kuhakikisha waandishi wa habari,watangazaji pamoja na wataalamu wa Teknolojia wanatumia vizuri Akili Mnemba kwaajili ya kuwasaidia na si kuwapotosha.

David Mwaluseke- DAR ES SALAAM

Waandishi wa habari pamoja na wasimamizi wa mtandao kutka vyombo mbalimbali vya habari nchini wamepewa elimu juu ya matumizi sahihi ya Akili Mnemba (AI) na DW Akademie ili kuhakikisha mitandao ya kijamii inabaki salama.

Mafunzo hayo yaliyofanyika ndani ya siku tano jijini Dar es salaam yalijikita katika kuhakikisha waandishi wa habari,watangazaji pamoja na wataalamu wa teknolojia wanatumia vizuri Akili Mnemba kwaajili ya kuwasaidia na si kuwapotosha.

Wakizungumza baadhi ya washikiri wa mafunzo hayo akiwemo Ally Choholo na Neema Swai wameishukuru DW Akademie kwakuandaa mafunzo hayo wakisema yatakwenda kuleta tija kwenye vyombo vyao.

Kwa upande wao wakufunzi akiwemo Moses Mutente, Elisha Simon pamoja na Warda Mansour wamewataka washiriki wa mafunzo hayo kuyatumia kwaajili ya matokeo chanya katika vyombo vyao vya habari.

Katika mafunzo hayo Radio kwizera iliwakilishwa na Pasensi Scarion Pamoja na David Mwaluseke ambapo mwishoni washiriki wote walitunukiwa vyeti vya mafunzo.

Mwandishi wa Habari wa Radio Kwizera Pasens Scarion (wa pili kutoka kulia) akikabidhiwa cheti baada ya mafunzo kutoka DW Akademie.
Mwandishi wa Habari wa Radio Kwizera, Davidi Mwaluseke (wa pili kutoka kulia) akikabidhiwa cheti baada ya mafunzo kutoka DW Akademie.