Radio Kwizera
Radio Kwizera
October 9, 2026, 3:15 pm

Amatus Chuchuba amewataka wahitimu kujisimamia wenyewe hasa kwa kipindi chote wawapo nyumbani kusubiri matokeo
Naomi Milton- KIGOMA.
Wazazi na walezi mkoani Kigoma wametakiwa kuacha tabia za kuwamilikisha wanafunzi simu wakati wawapo shuleni na likizo jambo linaloatihiri taaluma yao na kupelekea baadhi yao kufeli na kutofikia malengo waliyoyakusudia.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa shule ya Sekondari Mikamba Mwl. James Kivula wakati wa mahafali ya 8 ya kidato cha nne ya shule hiyo ambapo changamoto ya wanafunzi kumiliki simu ilitajwa kama chanzo cha kudhorofisha taaluma yao.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo Amatus Chuchuba ambaye ni madau wa elimu amewataka wahitimu kujisimamia wenyewe hasa kwa kipindi chote wawapo nyumbani kusubiri matokeo kwani mtaani vishawishi vipo vya Kila aina ni vyema Kila mwanafunzi akazingatia nidhamu aliyofundishwa akiwa shuleni.

Mwl. Agustino Lihaheja pamoja na wazazi waliohudhuria mahafali hayo wamesema wazazi wanapaswa kuwa mstari wa mbele katika kudhibiti matumizi ya simu kwa watoto kutokana na ukuaji wa Tekinolojia kwani baadhi Yao wamekuwa chanzo kwa kuwanunulia wao wenyewe jambo ambalo linapaswa kupigwa vikali na kuwaacha wasome Hadi hapo watakapojitambua.
