Radio Kwizera

Barabara ya mita 550 yajengwa, DC Muleba atoa onyo

November 21, 2026, 7:37 pm

Baadhi ya Viongozi wakiwa wameongozana na Mkuu Wilaya ya Muleba Dkt. Abel Nyamahanga (aliyevaa suti nyeusi) wakitembea katika barabara yenye urefu wa mita 550 iliyojengwa katika Kata ya Muleba. Picha na Shafiru Yusuph.

Dkt. Nyamahanga amesisitiza umuhimu wa wananchi kuheshimu maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya shughuli za Serikali

Na Shafiru Yusuph- Muleba, KAGERA

Wananchi wa Wilaya ya Muleba mkoani Kagera wametakiwa kuacha tabia ya kuvamia na kujenga katika maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya shughuli za Serikali.

Mkuu wa Wilaya ya Muleba, Dkt. Abel Nyamahanga, amesema hayo wakati wa hafla ya makabidhiano ya barabara ya lami yenye urefu wa mita 550 kwa wakazi wa Kitongoji cha Bukono, Kata ya Muleba iliyojengwa na ndugu Moses Kiduduye.

Dkt. Nyamahanga amesisitiza umuhimu wa wananchi kuheshimu maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya shughuli za Serikali ili kuwezesha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo bila vikwazo ikiwemo barabara.

Awali akisoma taarifa Meneja wa Wakala wa Barabara za Mjini na Vijijini Muhandis Dativa Telesphory amesema Barabara hiyo yenye urefu wa mita 550 na inatarajiwa kuchochea shughuli za kiuchumi kwa wakazi wa Kitongoji hicho.