Radio Kwizera

Mkataba wa Bil 5 wasainiwa kuondoa maji Bwawa la Katubuka, Kigoma

November 12, 2026, 1:35 pm

Mwonekano wa maji yakiwa ymafurika katika baadhi ya nyumba kwenye Bwawa la Katubuka mkoani Kigoma. Picha na Mtandao

Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Dkt Rashid Chuachua amemtaka mkandarasi kukamilisha kazi hiyo kwa wakati ili kuondoa adha kwa Wananchi.

Na Naomi Milton- KIGOMA.

Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji imesaini Mkataba wa ujenzi wa mfereji wa kuondoa maji bwawa la Katubuka na Kampuni ya Ujenzi ya ASABHI CONTRACTOR LIMITED kwa kushirikiana na PIONEER BUILDERS LIMITED ikiwa ni nyongeza ya mkataba uliogharimu shilingi Bilioni 5

Akizungumza katika hafla ya utiaji saini katika ukumbi Manispaa ya Kigoma Ujiji Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Dkt Rashid Chuachua amemtaka mkandarasi kukamilisha kazi hiyo kwa wakati ili kuondoa adha kwa Wananchi

Mkataba huo umesainiwa Kati ya Viongozi wa Kampuni ya ujenzi na Viongozi wa Halmashauri, Meya wa Manispaa ya Kigoma Ujiji Mussa Mauldi na Mkurugenzi wa Manispaa Mhandisi Juma Hamsini.

Aidha Mkandarasi anayetekeleza mradi huo Ibrahim Nyambacha amesema kuanzia sasa kazi itaanza na matarajio yao ni kuukamilisha mradi ndani ya siku 90 pekee.