Hatari ya maji yasiyotibiwa kwa binadamu-Kipindi
3 January 2025, 2:08 pm
Na Katalina Liombechi
Jamii imeshauriwa kutotumia maji yasiyotibiwa ili kuepuka magonjwa mbalimbali yanayotokana uchafu kama kipindupindu.
Mbonja Kasembwa ni Afisa Afya katika Halmashauri ya Mlimba Wilaya ya Kilombero ameiambia Pambazuko FM kuwa kumekuwa na utamaduni wa baadhi ya watu kutumia maji ya Mtoni kwa matumizi ya majumbani hali ambayo amesema inahatarisha afya zao kwani inaweza kupelekea magonjwa ya homa ya matumbo ,kichocho, safura, U.T.I na kuhara damu hivyo kujikuta wanaingia gharama kwa matibabu ya magonjwa yanayoweza kuepukika.
Aidha ameitaka jamii kujenga vyoo bora na kuacha kujisaidia hovyo kama vichakani na kwenye maeneo ya kingo za mito.
Katika hatua nyingine amesema wamekuwa wakishirikiana na RUWASA Kilombero kuweka dawa kila baada ya miezi mitatu katika visima rasmi vya jumuiya na vya watu binafsi ambapo hivi karibuni wameweka dawa vyanzo 1772.
KIPINDI:MATUMIZI YA MAJI MAJUMBANI