Zahanati Lumemo Kukamilika,Mwenyekiti aeleza
1 July 2021, 6:20 am
Na: Vitalisi Magalitele
Serikali ya Kijiji cha Lumemo kata ya Lumemo Wilayani Kilombero imeingiziwa fedha kiasi cha shilingi Milioni 15 kutoka Serikali ya Halmashauri ya mji wa Ifakara kwa ajiri ya kusaidia ujenzi wa Zahanati Kijijini humo
Akizungumza na pambazuko fm Juni 26 Ofisini kwake Mtendaji wa kijiji hicho Bw. Winfred Nanage amesema kutokana na changamoto iliyojitokeza ya ukosefu wa fedha ndio sababu kubwa ya kushindwa kumalizika kwa zahanati hiyo.
Hata hivyo amesema tayari hivi kalibuni Serikali ya halmaashauri ya mji wa ifakara imetoa fedha hizo ili kuunga mkono ujenzi wa zahanati hiyo na kwamba ili kutatua changamoto ya kituo cha Afya kijijini humo
Ameongeza kuwa wakati wowote kuanzia wiki ijayo yatatolewa matangazo ya kazi ili kuwapata wazabuni wa kusambaza vifaa pamoja na mafundi ujenzi mara tu baada ya kutolewa kwa muongozo wa matumizi ya fedha.
Hivyo Bw. Nanage amewataka wananchi wa kijiji hicho kujitokeza kwa wingi juni 28 siku ya juma 3 kwa ajiri ya kufanya usafi katika barabara iyendayo kwenye zahanati hiyo ambayo ipo katika kitongoji cha liala kijijini humo