Pambazuko FM Radio
Pambazuko FM Radio
5 December 2025, 1:12 pm

Kituo cha The Orbiti Day Care chafanya mahafali ya tatu; wazazi watakiwa kushiriki kikamilifu na kuboresha mazingira ya elimu kwa watoto.
Na; Isidory Mtunda
Kituo cha kulea watoto The Orbit Day Care, kilichopo kitongoji cha Uwanja wa Ndege, kata ya Kibaoni, Halmashauri ya Mji wa Ifakara mkoani Morogoro, kimefanikiwa kufanya mahafali ya tatu mwaka huu tangu kuanzishwa kwake, ambapo jumla ya watoto 15 (wavulana 10 na wasichana 5) wamehitimu elimu ya awali.
Mkuu wa kituo hicho, Madam Doreen Lasway, aliwataka wazazi kuendelea kushirikiana na kituo hicho kwa kuhudhuria vikao vinavyoitishwa na kulipa ada kwa wakati, kwasababu huduma zinazotolewa na kituo hicho ni bora ukilinganisha na gharama wanazotoa.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo, bwana. Jafari Iddy ambaye ni Mwenyekiti wa Huduma za Jamii kwa niaba ya Diwani wa Kata ya Kibaoni, alipokea changamoto ya uhaba wa magodoro na vifaa vya michezo. Ameeleza kuwa vifaa vya michezo vitatolewa mara shule zitakapofunguliwa, kwa mujibu wa diwani wa kata hiyo.

Aidha, alisisitiza umuhimu wa wazazi kuchangia huduma ya chakula kwa watoto wakiwa shuleni, akisema watoto wa madarasa ya chini hawapaswi kushinda njaa kwani inaweza kuathiri afya na maendeleo yao kielimu.
Mdau wa elimu na mzazi, Madam Faith Peter, amewasihi wazazi kutowaficha watoto nyumbani bali wawapeleke shule ili kuwapa msingi bora wa maisha, hasa kwa kuwa elimu ni hitaji la msingi hata katika kupata ajira.

Kwa niaba ya wazazi, Fatuma Mkilindi ametoa pongezi kwa walimu wa kituo hicho na kushauri kuboreshwa kwa zana za kufundishia ili kuchochea ari ya kujifunza kwa watoto na amesisitiza suala la ushirikiano kati ya walimu na wazazi hasa inapotokea wanahitajika.
sauti ya Fatuma Mkilindi