Pambazuko FM Radio

Miaka 15 ya SFUCHAS Wafanya upimaji bure

10 November 2025, 7:42 pm

Madaktari wa Chuo kikuu cha sayansu ya afya (SFUCHAS) katika huduma ya upimaji. Picha na Katalina Liombechi

Huduma hizi kiafya zmbazo zimetolewa ni sehemu ya maandalizi kuelekea maadhimisho ya miaka 15 ya kuanzishwa kwa Chuo cha SFUCHAS, kinachoendelea kuwa nguzo muhimu katika kutoa elimu na huduma bora za afya nchini

Na Katalina Liombechi

Kuelekea kumbukizi ya kuanzishwa kwa Chuo Kikuu cha Sayansi ya Afya Shirikisha cha Mtakatifu Fransisko– SFUCHAS, kinachotarajiwa kufanyika tarehe 15 Novemba mwaka huu, chuo hicho kimeanzisha kampeni maalum ya huduma za afya bure kwa wananchi wa Ifakara.

Kwa Mujibu wa Dkt. Claus Thomas Kaimu Mkurugenzi utafiti mahusiano na huduma za jamii SFUCHAS Huduma hizo zinatolewa kwa siku mbili kuanzia leo Novemba 10,2025 katika Zahanati ya Katindiuka, kwa ushirikiano kati ya Chuo cha SFUCHAS na Halmashauri ya Mji wa Ifakara.

Amesema Katika zoezi hilo Wananchi wanapata fursa ya kupimwa magonjwa mbalimbali kama vile uzito na urefu, kisukari, shinikizo la damu, maonesho ya huduma ya kwanza, ushauri kwa akina mama na watoto pamoja na kupata ushauri kwa ujumla wa kitaalamu kutoka kwa madaktari na wataalamu wa afya.

Dkt.Claus Thomas akieleza lengo la kutoa huduma ya vipimo. Picha na Katalina Liombechi
Sauti ya Dkt.Claus Thomas

Mkuu wa Wilaya ya Kilombero iliyopo mkoa wa Morogoro nchini Tanzania, Wakili Dunstan Kyobya, Akiwa katika zoezi hilo ametoa pongezi kwa chuo hicho na halmashauri kwa kuandaa huduma hizo zenye manufaa makubwa kwa jamii.

Amesema kampeni hiyo ni sehemu ya jitihada za serikali na taasisi binafsi katika kuboresha afya za wananchi, huku akiwahamasisha wakazi wa Katindiuka na maeneo jirani kujitokeza kwa wingi kupata huduma hizo.

Mkuu wa wilaya ya kilombero Mh. Kyobya. Picha na Katalina Liombechi
Sauti ya DC Kyobya

Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Katidndiuka Dkt. Magreth Mwaisaka amesema kuna kila sababu wananchi kunufaika na huduma za afya zinazotolewa katika zahanati hiyo kutokana na fursa hiyo na hata baada ya zoezi hilo.

Mganga Mfawidhi Zahanati ya Katindiuka. Picha na Katalina Liombechi
Sauti ya Mganga Mfawidhi Zahanati ya Katindiuka

Baadhi ya wa wananchi waliojitokeza katika huduma hiyo ya upimaji bure wameeleza kuwa ni bahati kwao kufikiwa katika maeneo yao huku wakitoa wito kwa wananchi wenzao kuchangamkia fursa hiyo na kuachana na mawazo potofu.

Pendo Edward mmoja kati ya waliojitokeza kupima afya. Picha na Katalina Liombechi
Sauti ya Wananchi waliojitokeza