Pambazuko FM Radio

Watu wenye ulemavu wasisitizwa kujishughulisha

13 June 2025, 12:13 pm

Picha ya Lucas Ngajimala akitengeneza sabuni ya maji (Picha na Katalina Liombechi)

Kuomba huku ni kitu kibaya sana nikaona bora nipambane

Na Katalina Liombechi

Inaelezwa kuwa katika jamii nyingi, watu wenye ulemavu hukumbana na mitazamo potofu ambayo huwakatisha tamaa katika maisha ya kila siku.

Hayo yamebainika baada ya Pambazuko FM kuzungumza na Lucas Ngajimala Mkazi wa Mtaa wa Uwanja wa Taifa A Kata ya Viwanjasitini Halmashauri ya Mji wa Ifakara  mjasiriamali mwenye ulemavu wa viungo ni mmoja wa waliothubutu kuvuka vizingiti hivyo na sasa amekuwa kama mfano wa kuigwa kwa wengine wenye changamoto kama yake.

Lucas ameeleza kuwa alipata ulemavu baada ya kuanguka kutoka kwenye mnazi, lakini hali hiyo haikumzuia kuendeleza maisha Kwa sasa anajishughulisha na utengenezaji wa sabuni za maji kazi ambayo amesema imemwezesha kujitegemea na kuendesha maisha yake bila kutegemea kuomba omba.

Sauti ya Lucas Ngajimala Mjasiliamali

Hata hivyo, ameiomba serikali pamoja na wadau mbalimbali kumsaidia kupata toyo ya umeme ambayo itamwezesha kusambaza bidhaa zake kwa ufanisi zaidi pia kupata Ofisi kwani kwa sasa analazimika kutengeneza sabuni kwenye chumba anacholala kitu ambazo haishauriwi kiafya na kwamba yeyote anayeguswa kumsaidia awasiliane kupitia nambari ya 0767429446.

Picha ya Lucas Ngajimala Mjasiliamali(Picha na Katalina Liombechi)
Sauti ya Lucas Ngajimala

Lucas ametumia fursa hiyo kuwahamasisha watu wengine wenye ulemavu akisisitiza umuhimu wa kujishughulisha na shughuli za ujasiriamali badala ya kuombaomba mitaani huku akionesha wasiwasi wake juu ya changamoto zinazokumba watu wenye ulemavu kwani amesema wengi wao wamekuwa wakishindwa kufuatilia mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri kwa wanawake, vijana na wenye ulemavu kwa kuhofia usumbufu.

Sauti ya Lucas Ngajimala

Kwa upande wao Maafisa maendeleo ya Jamii katika Halmashauri ya Mji wa Ifakara wakizungumza na Pambazuko FM hivi karibuni Charles Chali na Esther Mtweve wamewaondoa shaka watu wenye ulemavu kwamba hakuna usumbufu kufuatilia mikopo hiyo na kwamba kwasasa idara yao imeenda mbali zaidi kuwafikia katika kata zao.

Picha ya Charles Chali Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Mji wa Ifakara(Picha na Katalina Liombechi)
Sauti za Maafisa maendeleo ya jamii Halmashauri ya Mji wa Ifakara

Naye Mkuu wa Idara hiyo Bi Florence Mwambene ameelezea fursa ya kunufaika na mikopo ya Asilimia 10 kwa makundi yote yanayolengwa na mkopo huo.

Picha ya Bi Florence Mwambene Mkuu wa Idara ya Maendeleo (Picha na Katalina Liombechi)
Sauti ya Bi Florence Mwambene Mkuu wa Idara maendeleo ya Jamii