Pambazuko FM Radio

TFS kuokoa bonde la Kilombero kwa kutunza misitu ya asili, upandaji miti

21 March 2025, 4:35 pm

Picha ya Mhifadhi TFS wa kwanza kulia katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Kilombero(Picha na Kuruthumu Mkata)

Na Katalina Liombechi/Kuruthumu Mkata

Wakala wa huduma za Misitu Tanzania TFS Wilaya ya Kilombero Wajielekeza katika kuokoa bonde la Kilombero kwa kutunza misitu ya asili na kurithisha utamaduni wa Kupanda miti kwa uendelevu wa Rasilimali mbalimbali.

Mhifadhi Misitu Wilaya hiyo Zarina Sheweji Haridi ameyasema hayo hii leo March 21,2025 katika Maadhimisho ya Siku ya upandaji miti Kitaifa ikiwa ni siku pia ya Misitu Duniani ambapo Wilayani kilombero Siku hiyo inaadhimishwa kwa kupanda miti 75,000 kwenye maeneo ya Umma kama mashuleni,zahanati na maeneo mbalimbali ya watu binafsi.

Mhifadhi huyo wakati akipanda mti katika shule ya Sekondari Ihanga ameeleza kuwa hali ya Uhifadhi wa Misitu kwa sasa katika Wilaya ya Kilombero imeimarika kutokana na Elimu ya shughuli mbadala kwa jamii,kuhamasisha upandaji miti na doria za mara kwa mara hivyo kusaidia watu kuacha utegemezi wa rasilimali misitu kujipatia kipato.

Sauti ya Mhifadhi Misitu TFS Kilombero

Katika Maadhimisho hayo Mgeni rasmi ni Mkuu wa Wilaya ya Kilombero wakili Dunstan Kyobya ambaye mara kadhaa amekuwa akisisitiza usimamizi endelevu wa Misitu na kuhamasisha kampeni ya soma na mti,Ishi na Mti.

Picha ya Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Wakili Dunstan Kyobya(picha na Kuruthumu Mkata)

Kauli mbiu Siku ya Upandaji Kitaifa mwaka huu yanakwenda na kauli mbiu isemayo “Ongeza thamani ya mazao ya misitu kwa uendelevu wa rasilimali za misitu kwa manufaa ya kizazi cha sasa na Kijacho”

Maadhimisho haya yanafanyika kwa lengo la Kuhamasisha hifadhi ya Misitu, Kupambana na Mabadiliko ya Tabianchi,Kuongeza Ufanisi wa Upandaji Miti,Kuongeza Uelewa kuhusu Umuhimu wa Misitu kwa Uchumi Pamoja na Kuhamasisha ushirikiano katika Ulinzi wa Mazingira.