Pambazuko FM Radio
Pambazuko FM Radio
13 February 2025, 9:38 pm
Na Katalina Liombechi
Wakala wa huduma za Misitu Tanzania TFS Wilaya ya Kilombero imesema kuwa Radio imekuwa na Mchango mkubwa katika kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia nchi.
Hayo ni kwa Mujibu wa Mhifadhi Daraja la Kwanza Kutoka mamlaka hiyo Shukrani Madinda wakati akizungumza na Radio Pambazuko FM Ofisini kwake.
Mhifadhi huyo amesema kupitia radio wamekuwa wakielimisha jamii kuhusu shughuli za Uhifadhi hasa kutunza rasilimali misitu,kuelimisha njia mbadala za kiuchumi na Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia ili kupunguza Uharibifu katika maeneo yaliyohifadhiwa ili kufanya maisha kuwa endelevu.

Hata hivyo baadhi ya Wananchi Katika Mtaa wa Uwanja wa Taifa A Halmashauri ya Mji wa Ifakara wameelezea maoni yao juu ya Mchango wa Radio .
Ikumbukwe kuwa Siku ya Radio Duniani huadhimishwa kila ifikapo February 13, ambapo kwa mwaka huu maadhimisho hayo yamebeba kauli mbiu ya “RADIO NA MABADILIKO YA TABIANCHI”