Pambazuko FM Radio

Madiwani Ifakara watoa maagizo watoto kutembea umbali mrefu kufuata elimu­

13 February 2025, 9:28 pm

Na Katalina Liombechi

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Ifakara Mh.Kasim Nakapala ameiagiza Ofisi ya Mkurugenzi kumaliza mchakato wa Ukaguzi wa Jengo la shule ya Sekondari na Amali ya Mpanga Iliyopo Kata ya Kisawasawa ili watoto waanze kuripoti kuanza masomo.

Maagizo hayo yanakuja baada ya Mh.Songo Daniel Diwani wa Kata hiyo kuuliza swali la Papo kwa hapo kuhusu muda gani watoto wataripoti kuanza masomo katika shule hiyo Kutokana na ujenzi wake kukamilika?

Mh.Songo katika kikao hicho cha kawaida robo ya pili cha Baraza la Madiwani ambacho kimeketi Feb 12,2025 katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mlimba uliopo Ifakara,ameeleza kuwa Idadi ya watoto waliochaguliwa katika shule hiyo kwa mwaka huu ni 69 kutoka vijiji vya mikoleko na Mpanga ambapo kwasasa bado wanaendelea kupata changamoto ya kutembea umbali mrefu kufuata elimu katika Shule mama ya Sekondari Kisawasawa.

Sauti ya Diwani Songo Daniel
picha ya Diwani Songo Daniel(picha na Katalina Liombechi

Kwa mujibu wa Kaimu Afisa elimu Sekondari Hadinani Ungite katika majibu yake amesema Mchakato uliosalia ni Wadhibiti Ubora kukagua Majengo,kuitisha kikao na wazazi na baadaye watoto kutakiwa kuripoti ikiwa ni Mchakato unaofanyika ndani ya Muda Mfupi.

picha ya Kaimu afisa Elimu Sekondari Hadinani Ungite(picha na Katalina Liombechi)
sauti ya Hadinani Ungite

Kufuatia majibu hayo Mwenyekiti Mh.Nakapala ameelekeza Mchakato huo ufanyike haraka ili hadi kufikia Feb 19,2025 watoto hao wawe wamesharipoti.

Sauti ya Mwenyekiti wa Halmashauri Mh.Nakapala

Kumbuka Ujenzi wa Shule ya Mpanga umegharimu kiasi cha Tsh.Mil 528 Fedha kutoka Serikali kuu ambapo imekusudiwa kutoa masomo ya Sekondari na ufundi.