Ushirikiano AWF, wadau kuhamasisha uwekezaji kimkakati Kilombero
28 December 2024, 7:22 pm
Na Katalina Liombechi
Katika kukabiliana na changamoto za shughuli za kibinadamu zinazohatarisha upotevu wa Bionuwai na Mabadiliko ya tabianchi mashirika ya kimataifa na ya kikanda kama African Wildlife Foundation (AWF) yamejizatiti kutafuta suluhisho endelevu.
Mchumi Kilimo kutoka AWF Alexander Mpwaga akizungumza katika tamasha Kilombero lililofanyika hivi karibuni katika Viwanja vya CCM Tangani amemweleza Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Wakili Dunstan Kyobya kuwa Mojawapo ya mikakati muhimu ya Kufanya Uhifadhi na uwekezaji endelevu ni kushirikiana na wadau mbalimbali, ikiwa ni pamoja na serikali, jamii za wenyeji, taasisi za kifedha, na mashirika yasiyo ya kiserikali, ili kuhakikisha kuwa juhudi za uhifadhi zinazoanzishwa ni endelevu na zinajenga mazingira bora kwa wanyamapori na binadamu.
KIPINDI:USHIRIKIANO AWF NA WADAU KUHAMASISHA UWEKEZAJI KIMKAKATI.