Pambazuko FM Radio
Mavuno na hifadhi ya kokoa-Kipindi
27 December 2024, 2:44 pm
Na Katalina Liombechi
Wakulima wa Kokoa wameshauriwa kuzingatia uvunaji na uhifadhi mzuri wa Kokoa ili mazao yaweze kukubalika sokoni.
Kwa mujibu wa Afisa Kilimo Mratibu wa zao la Kokoa Halmashauri ya Mlimba Dismas Charles Amri amesema katika kuvuna kokoa kuna hatua tofauti tofauti na vifaa maalumu ikiwa ni pamoja na kuvuna kwa kutumia kisu kikali,kuvundika kwa kuweka kwenye box maalumu kwa muda wa siku 6 kwa maelekezo ya kitaalamu.
KIPINDI:MAVUNO NA HIFADHI YA KOKOA