Pambazuko FM Radio

Six rivers Africa waokoa hifadhi wakabidhi miradi mbadala kwa wananchi-Ifakara

16 December 2024, 8:29 pm

Na Katalina Liombechi

Shirika la six Rivers Afrika wamekabidhi Miradi ya kufuga nguruwe na Kuuza Unga wa Sembe yenye thamani ya shilingi Mil.7 kwa vikundi viwili kutoka Kata za Katindiuka na Kibaoni katika Halmashauri ya mji wa Ifakara ikiwa ni miongoni mwa Maeneo yaliyopakana na Hifadhi ya Nyerere.

Awali akizungumza hii leo Desemba 16,2024 Akiwa katika kata ya Katindiuka Mratibu wa Miradi kutoka Shirika hilo Irene masonda amesema mradi huo ni kutokana na uhitaji wa kikundi cha Upendo,nao ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu ya kiuhifadhi ya kuwawezesha kiuchumi jamii zinazopakana na hifadhi ni mradi ambao umegharimu kiasi cha shilingi Mil 3.5.

Picha ya Irene Masonda Afisa Miradi Shirika la Six rivers Africa(Picha na Katalina Liombechi)
Sauti ya Irene Masonda Afisa Miradi Shirika la Six rivers Africa

Afisa Mifugo Kata ya Katindiuka Amesema Mradi huo unakwenda kubadili maisha ya kikundi hicho kwani ni nguruwe wa kisasa na wanahitajika Sokoni.

Picha ya Steven Muyoya afisa mifugo kata ya katindiuka(Picha na katalina Liombechi)
Sauti ya Steven Muyoya afisa mifugo kata ya katindiuka

Mmoja kati ya wanakikundi amelishukuru shirika la Six rivers na kwamba wameendelea kuona umuhimu wa eneo lao kupitiwa na hifadhi kutokana na fursa wanazopata na wanazozitazamia kuzipata.

Sauti ya Herieth Mtama Mwanakikundi cha Upendo Katindiuka

Aidha katika hatua nyingine Six Rivers Afrika wakikabidhi Mradi wa Biashara ya kuuza unga wa sembe kwa kikundi cha Nguvu moja kilichopo katika kijiji cha Lungongole Kata ya Kibaoni amesema nao ni mradi wenye thamani ya Shilingi Mil 3.5 utakaowasaidia kujikwamua kiuchumi na kuacha kutegemea rasilimali kutoka hifadhini kujikimu kimaisha.

Sauti ya Irene Masonda Afisa Miradi Shirika la Six rivers Africa
Picha ya Irene Masonda afisa miradi Six rivers africa kaikabidhi unga wa sembe(picha na katalina Liombechi

Akizungumza wakati wa kukabidhi Afisa Maendeleo kata hiyo Esther Mtweve amesema imani yake ni kwamba wanakikundi hao watakwenda kutekeleza mradi huo kwa uaminifu mkubwa.

Picha ya Esther Mtweve afisa maendeleo ya jamii kata ya kibaoni(Picha na Katalina Liombechi)
Sauti ya Esther Mtweve afisa maendeleo ya jamii kata ya kibaoni

Baadhi ya wanakikundi cha Nguvu moja kijiji cha Lungongole Wamesema wataendesha mradi huo kwa namna ya kujenga uaminifu ili vijana wengine  na jamii kwa ujumla waweze kunufaika kama wao walivyopata fursa hiyo huku mmoja wa wanakikundi akieleza kuachana na shughuli ya kukata miti kwa ajili ya biashara ya Mkaa ambapo amekiri imeathiri mazingira na afya yake.

Picha ya Wanakikundi cha Nguvu moja kijiji cha Lungongole Kata ya kibaoni(picha na Katalina Liombechi)
Sauti za Wanakikundi cha Nguvu moja kijiji cha Lungongole Kata ya kibaoni