Pambazuko FM Radio

Vinara uhifadhi mazingira, utalii wakumbukwa na AWF Kilombero

5 December 2024, 11:45 am

Na Katalina Liombechi

Katika jitihada za kuendelea kuokoa na kulilinda Bonde la Kilombero Mfuko wa Uhifadhi wa Wanyamapori Afrika AWF Wakabidhi Mfano wa hundi zaidi ya Tsh.Mil 90 Kwa Vinara wa Uhifadhi kurejesha Mazingira ya asili kutangaza Utalii.

Fedha hizo zimekabidhiwa kwa wadau wa vinara wanne wa uhifadhi katika hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Twiga Hotel Tarafa ya Mang’ula wilayani Kilombero katika Mkoa wa Morogoro.

Akikabidhi fedha hizo Mgeni rasmi Katika hafla hiyo Katibu tawala Msaidizi Mkoa wa Morogoro Dkt.Rozaria Rwegasira amewapongeza AWF Kwa kubuni njia ya kushirikisha wadau wengine kutekeleza shughuli za uhifadhi huku akiwataka Vinara waliopatiwa fedha hizo kuzitumia kwa malengo kusudiwa kwa Maslahi mapana ya Taifa la Tanzania.

Picha ya mgeni rasmi Katibu tawala msaidizi Mkoa wa Morogoro Dkt.Rozaria Rwegasira(Picha na Katalina Liombechi)
Sauti ya Katibu tawala msaidizi Mkoa wa Morogoro Dkt.Rozaria Rwegasira

Kwa mujibu wa Mchumi Kilimo wa AWF Alexander Mpwaga amesema matarajio yao kuona wanapata Masuluhisho ya Asili na kujibu changamoto kiuhifadhi ili Bonde la kilombero liendelee kubaki salama wakati huo uchumi wa watu ukiwa umeimarika.

Sauti ya Mchumi Kilimo kutoka AWF Alexander Mpwaga

Wakizungumza baada ya kupokea Fedha hizo Viongozi hao vinara kutoka Association Mazingira,Kilombero group for community development (KOCD),Mazingira ni uhai Foundation na Hifadhi ya jamii ILUMA (ILUMA WMA)wameishukuru AWF kuwaamini na kwamba watafanya kwa mujibu wa makubaliano.

Picha za Vinara wa Uhifadhi Bonde la Kilombero(Picha na Katalina Liombechi)
Sauti za Vinara wa Uhifadhi Bonde la Kilombero

Kumbuka fedha iliyokabidhiwa Desemba 2,2024 kwa kila taasisi ni Zaidi ya Tsh.Mil.24 ambayo inakwenda kutekeleza Miradi kwa kipindi cha mwaka 1 nikuongeza uzalishaji wa zao la Kokoa katika Halmashauri ya Mlimba, kuviwezesha vikundi vya ufugaji nyuki katika eneo la Vidunda,kurejesha Mto Ikwambi pamoja na kufanya Mbio za hisani kutangaza Utalii kuelezea umuhimu na Makusudi ya kuifanya hifadhi hiyo ya jamii kuwa endelevu.