Pambazuko FM Radio

Kipi kimeathiri ubora mto Mchombe?-Kipindi

21 October 2024, 1:28 pm

AWF wamekuwa wakishirikana na Jumuiya za watumia maji kufanya tathmini ili kuona njia bora ya kufanya ubora wa Mto unaongezeka.

Na Katalina Liombechi

Mfuko wa Uhifadhi wa Wanyamapori Afrika AWF wameshirikiana na Jumuiya ya Watumia Maji Bonde Dogo la Mto Mngeta Chini kufanya tathmini ya ubora na afya ya mto Mchombe ili kuona namna ya kuendelea kuutunza Mto huo.

Akizungumza mara baada ya tathmini hiyo imefanyika kwa kutumia mbinu ya kibaiolojia kwa kupima wadudu wanaopatikana ndani ya mto katika maeneo ya mchanga, nyasi na mawe, mhifadhi kutoka AWF Antidius Raphael amesema wamebaini kuwa afya na ubora wa mto huo imeshuka kutoka daraja B hadi C huku akieleza kuwa dhana shirikishi ndiyo njia itakayosaidia kufanya mto huo kubaki salama.

KIPINDI KUHUSU TATHIMININI YA UBORA WA MTO MCHOMBE