STEP yawahimiza vijana katika shughuli za uhifadhi wa tembo Kilombero
9 October 2024, 12:23 pm
Na Henry Bernad Mwakifuna
Shirika linalojihusisha na Uhifadhi wa Tembo Kusini mwa Tanzania STEP limeendelea kuwahimiza Vijana kuona umuhimu wa uhifadhi na kuitumia Fursa ya uwepo wa Vivutio mbalimbali vilivyomo ndani ya Wilaya ya Kilombero ili waweze kunufaika Zaidi kupitia Sekta hiyo.
Mratibu wa Mradi Mahusiano ya Tembo na Watu wa Shirika hilo Wilaya ya Kilombero Catherine Kimario ameyasema hayo katika Fainali ya TEMBO CUP Msimu wa Pili iliyofanyika katika Viwanja vya Msolwa Ujamaa Tarafa ya mang’ula lengo likiwa ni kuendelea kutoa Elimu ya Uhifadhi wa Tembo na kuishirikisha jamii katika kumuhifadhi Mnyama huyo.
Amesema kama STEP licha ya Kufanya michezo pia Wamekuwa wakifanya mambo mbalimbali ikiwa ni Pamoja na kuwezesha Wakulima kikundi cha ufugaji wa nyuki na kwamba wamekuwa wakishirikiana na Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Udizungwa katika kutoa Elimu ya Uhifadhi kwa wanafunzi,Vijana na makundi mbalimbali.
Mgeni rasmi Afisa Mtendaji Kata ya Mwaya Acrey Mhenga akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Ifakara Bi Zahara Michuzi amesema kuwa kumlinda Mnyama Tembo imeleta fursa hiyo ya kimichezo kwa Vijana hivyo kwa Kulinda Shoroba itasadia kufanya Uhifadhi kuwa Endelevu na Wadau hao kuendelea zaidi kusaidia katika shughuli mbalimbali za Kijamii ikiwa ni pamoja na Michezo hiyo.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Msolwa ujamaa ameishukuru STEP Kwa Bonanza hilo huku akiwataka Vijana kutumia fursa hiyo kujiendeleza zaidi kimichezo kwani amesema Michezo ni Ajira.
Mashindano ya TEMBO CUP yalihusisha Timu 22 na Fainali imefanyika Oktoba 1,2024 ambayo imehusisha timu ya Nyange&Msolwa Stesheni ambapo Nyange imeibuka Mshindi wa Bao 1-0 hivyo kujipatia Kombe Fedha kiasi cha Tsh.800,000/= na Mpira Mmoja huku Mshindi wa Pili wakipata kiasi cha Tsh.600,000/= na Mpira.