Pambazuko FM Radio

Uvuvi haramu unahatarisha mazalia ya samaki-Kilombero

17 July 2024, 7:12 pm

Na Katalina Liombechi

Inaelezwa Kuwa Uvuvi Haramu unahatarisha Mazalia ya Samaki hali inayoweza kusabibisha kukosa uendelevu wa Rasilimali hiyo.

Afisa Mifugo Halmashauri ya Mji wa Ifakara Dkt Dunia Mlanzi amesema kumekuwa na Watu wanaotumia dhana mbalimbali zisizo halali katika uvuvi ambapo kwenye hilo wamekuwa wakishirikiana na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA.

Aidha Dkt Dunia amesema njia Pekee ya kuondokana na Adha hiyo ni Kufanya Uvuvi Wenye tija kwa kuvua kisasa na kufanya Ufugaji wa Samaki kwa Kujenga Mabwawa kisasa hivyo kupunguza Utegemezi wa Rasilimali hiyo kutoka Kwenye Vyanzo vinavyohifadhiwa huku wakinufaika Kiuchumi.

Hata hivyo kwa Mujibu wa Wataalam Uvuvi wa kisasa unajumuisha mbinu mbalimbali za kisasa na teknolojia zenye lengo la kuboresha ufanisi, tija na uendelevu wa shughuli za uvuvi Mbinu hizi ni pamoja na Uvuvi kwa kutumia boti za kisasa, Uvuvi kwa kutumia nyavu za kisasa,Ufuatiliaji wa samaki,Ufugaji wa samaki na kutumia Teknolojia.

Kipindi kuhusu uvuvi wenye tija