Wafugaji watakiwa kufuga kisasa kuongeza tija
14 July 2024, 5:42 pm
Na Katalina Liombechi
Wafugaji wanashauriwa kufuata sheria na kanuni zote zinazohusiana na ufugaji wa wanyama ili kupata tija.
Akizungumza na Radio Pambazuko FM Daktari wa Mifugo kutoka Halmshauri ya Mji wa Ifakara Dunia Mlanzi amesema ili mfugaji apate tija anatakiwa kuzingatia mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwa na eneo la kujenga banda bora, mbegu bora ya mifugo, malisho, namna bora ya kudhibiti magonjwa kwa mifugo kwa kutumia madaktari wanaotambulika.
Hata hivyo inashauriwa kuwa ufugaji wa wanyama kwa tija unaweza kuwa shughuli yenye faida sana kwa kufuata miongozo, unaweza kuboresha tija ya wanyama wako, kuongeza mapato yako na kuchangia katika maendeleo ya uchumi wa Tanzania. Pata vibali vinavyohitajika kwa ufugaji wa wanyama, shiriki katika mafunzo na semina kuhusu ufugaji bora wa wanyama.
Kipindi kuhusu Ufugaji wa wanyama kwa tija.