Pambazuko FM Radio

AWF yakabidhi vifaa kuendesha kilimo cha parachichi Kilosa-Kipindi

13 July 2024, 10:17 am

Na Katalina Liombechi

Wananchi wa kata ya Vidunda wilayani Kilosa wanatarajia kunufaika kupitia zao la parachichi ikiwa ni zao la kimkakati mkoani Morogoro.

Mchumi Kilimo kutoka Mfuko wa Uhifadhi wa Wanyamapori Afrika AWF Alexander Mpwaga amezungumza hayo wakati akikabidhi vifaa mbalimbali vyenye thamani ya Sh Mil 62 vitakavyosaidia kuendeleza vitalu vya miche ya parachichi katika vijiji vya Chonwe, Udung’u na Vidunda  ambapo wanatarajia wananchi wa maeneo hayo wataacha utegemezi wa rasilimami zilizohifadhiwa wakati huo uchumi wao ukiimarika.

Hata hivyo kwa mujibu wa wataalam, kilimo cha zao la parachichi kinasaidia udhibiti wa mmomonyoko wa udongo, uhifadhi wa vyanzo vya maji, kupunguza uchafuzi wa hewa, kuongeza viumbe hai, kuboresha ubora wa udongo, kupunguza matumizi ya mbolea za kemikali na kuongeza mapato ya wakulima.

Kipindi kuhusu kilimo cha zao la parachichi kudhibiti mmomonyoko wa udongo.