TFS Kilombero yapanda mizanzibari 100 katika shule ya msingi Kiogosi
28 May 2024, 11:09 am
Mhifadhi Shukurani Madinda akiwa na wanafunzi wa S/M Kiogosi Ifakara- Picha na Isidory Matandula
Wakala wa misitu Tanzania,wamekuwa wakijishughulisha na shughuli mbali mbali ikiwemo upandaji wa miti kwenye shule, taasisi na kufanya doria katika maeneo ya hifadhi ili kudhibiti majangili wanaokata miti ovyo.
Na; Isidory Matandula
Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) leo wamepanda miche ya miti 100 aina ya Mizanzibari katika shule ya Msingi Kiogosi, kata ya Lumemo, halmashauri ya mji wa Ifakara, mkoani Morogoro.
Akizungumza na Pambazuko fm baada ya zoezi hilo, mhifadhi Shukurani Madinda, amesema miti hiyo itasaidia wanafunzi hao kwaajili ya kivuli wakati wa kujisomea na hewa ya Oksijeni.
Mhifadhi Madinda na mwanafunzi wa S/M Kiogosi wakipanda mti wa Mzanzibari – Picha na; Isidory Matandula
sauti ya mhifadhi Shukurani Madinda
Kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule hiyo, Nasoro Mbalikila, amewashukuru wakala hao, kwani miti hiyo itawasaidia wanafunzi kwa kivuli wakati wa kujisomea.
Mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Kiogosi Mwl Mbalikila – picha na Isidory Matandula
Sauti ya mwl mkuu Mbalikila
TFS imekuwa na utaratibu wa kupanda miti katika taasisi mbali mbali, ambapo mwaka jana katika shule hiyo walitoa miche ipatayo miatano.