Wanufaika wa Tasaf walia kuondolewa kwa ruzuku-Ifakara
18 February 2023, 1:18 pm
Na Elias Maganga
Wanufaika wa mfuko wa maendeleo ya Jamii Tasaf awamu ya tatu Kata ya Mbasa katika Halmashauri ya Mji wa Ifakara wamekuwa na hali ya sintofahamu juu ya ruzuku ya msingi na utekelezaji wa mradi wa barabara huku baadhi ya wanufaika wakisitishiwa malipo.
Wakizungumza na Pambazukofm baadhi ya wanufaika wa mfuko wa maendeleo ya jamii Tasaf awamu ya tatu,wamesema awali walielezwa kuwa miradi ya jamii inayotekelezwa na wanufaika hao,ambapo kimsingi malipo yake ni shilingi elfu tatu kwa siku wanashangazwa kuondolewa kwa ruzuku ya shilingi 24000 ambayo huwa wanalipwa baada ya miezi miwili.
Akitolea ufafanuzi Mratibu wa mfuko wa maendeleo ya jamii Tasaf kwa ngazi ya Halmashauri ya mji wa ifakara Bi Brigita Haule amesema kuwa kwasasa wako katika awamu ya tatu ya utekelezaji wa mpango wa kunusuru kaya masikini katika awamu hii tasafu imejikita sana kutoa ruzuku kwa wananchi wenye hali duni kimaisha na kwa kata ya Mbasa wanatekeleza mradi wa Barabara
Habari zingine kutoka Pambazuko FM
Mikakati ya kuondokana na uchafu wa mazingira yaanza kutekelezwa-Ifakara
Zoezi la uondoaji Mifugo limeanza katika Bonde la Mto Kilombero
Kuhusu kuondolewa kwa ruzuku kwa baadhi ya wanufaika wa Tasaf,Bi Brigita amesema kaya yoyote inayotakiwa kufanya kazi katika mradi wa barabara kuna sehemu ya ruzuku inasitishwa
Baadhi ya wanufaika kuondolewa kwenye mpango huo wa kunusuru kaya masikini Bi Brigita amekanusha na kusema hakuna mtu aliyeondolewa kwenye mpango huo isipokuwa kuna baadhi ya wanufaika wamesitishiwa malipo na hiyo inatokana na sababu mbalimbali ikiwemo ya mlengwa kutofika kwenye kituo cha kupokelea malipo,kifo na wale wanaostahili kufanya kazi za miradi ya kijamii.
Ikumbukwe kuwa Kipindi cha Pili awamu ya tatu wa mpango wa kunusuru kaya masikini kitafikia malengo yake kwa kutekeleza shughuli mbali mbali kupitia sehemu kuu tatu ambazo ni uhawilishaji fedha ambao utaongeza kipato cha kaya na kuwekeza katika afya na elimu ya watoto, kuinua uchumi wa kaya kwa kujenga uwezo kwa kaya katika utunzaji rasilimali na kutengeneza njia mbadala na endelevu za ajira na kushiriki katika kazi za jamii na kupata kipato cha ziada kwa matumizi ya kaya kama chakula na kugharamia mahitaji mengine ya msingi na wakati huo wakiboresha miundombinu katika jamii na kupata ujuzi na stadi za maisha.