Pambazuko FM Radio

Zoezi la uondoaji Mifugo limeanza katika Bonde la Mto Kilombero

10 February 2023, 4:24 pm

Kikosi kazi cha vyombo vya ulinzi na usalama Wilayani Kilombero wakiwa kwenye Operesheni ya kuondoa mifugo{Picha na Kuruthum Mkata}

Na Kuruthum Mkata

Operesheni ya kuondoa Mifugo ndani ya Bonde la Mto Kilombero, limeanza kutokana na maagizo ya Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Wakili Dunstan Dominick Kyobya imeanza katika Kijiji cha Merera,Kata ya Chita ,Tarafa ya Mngeta, Halmashauri ya Wilaya Mlimba.

Zoezi limeanza Februari 9 mwaka huu na tayari kikosi kazi cha vyombo vya ulinzi na usalama viko katika eneo husika na wameanza katika Kambi ya Barafu na kambi ya Bata.

Kwa mujibu wa tarifa imeeleza kuwa kikosi kazi kimefanikiwa kuwakamata wakulima 10 waliolima ndani ya hifadhi ya Bonde la Mto Kilombero  na Ng’ombe 203 na operesheni hiyo ni endelevu

Wakulima waliokamatwa kwenye hifadhi ya Bonde la mto Kilombero{picha na Kuruthum Mkata}

Agizo la kuwataka wafugaji waondoke ndani ya Bonde hilo alilitoa februari 2 mwaka huu alipokuwa kwenye ziara ya kikazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba ambapo aliwasisitiza kuwa bonde hilo ni mahususi kwa ajili ya uhidadhi.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Wakili Dunstan Kyobya akisistiza kuondoka kwa wafugaji katika Bonde la Mto Kilombero

 Ikumbukwe kuwa Januari 18 mwaka huu Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Bi Fatma Mwassa wakati akizindua zoezi la upandaji miti katika Halmashauri ya Mji wa Ifakara Wilayani Kilombero alitoa maagizo ikiwa ni pamoja na wafugaji kuondoka kwenye eneo la Bonde la Mto Kilombero.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Bi Fatma Mwassa{Picha kwa hisani ya Mwananchi communication}
Sauti ya Mkuu wa Mkoa w Morogoro Bi Fatma Mwassa akizungumza wakati wa uzinduzi wa zoezi la upandaji Miti katika Halmashauri ya mji wa Ifakara naye akisisitiza kuondolewa kwa wafugaji