Wananchi Watakiwa Kuchangia Maendeleo ya Shule
25 June 2021, 5:51 am
Na:Katalina Liombechi
Wananchi wa Kata ya Igawa katika Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi wameombwa wawe na Utaratibu wa kuchangia michango ya Shule bila kujali kuwa ana au hana Mtoto anayesoma katika shule husika.
Kauli hiyo imetolewa na Diwani wa Kata ya Igawa bwana SEVELUSI AMAN KAMGUNA Wakati anazungumza na Pambazuko Fm ilipotaka kujua juu ya miradi ya shule hususan katika upande wa Elimu.
Diwani KAMGUNA amebainisha njia bora ya Kuanzisha vyanzo vya Mapato katika Kata ni Kushirikisha Jamii na Wadau mbalimbali wa Elimu ili kupata Mawazo na Maoni juu ya uanzishwaji wa Vyanzo hivyo huku akitaja chanzo Kikuu cha Mapato kwa sasa katika Shule zake ni Kilimo.
Mratibu wa Shirika lisilo la Kiserikali linalojishughulisha na Masuala ya Elimu na Mazingira la Save Education and Future Development foundation Bwana Clarensi Mosha amesema Shirika hilo liko tayari kushirikiana uongozi wa kata hiyo ili kuwapatia mawazo ya kubuni vyanzo vya Mapato yakayowezesha kukuza Elimu katika Kata hiyo
Neema Taita na Tasibu Abeid ni Miongoni mwa Wananchi waishio katika Kata hiyo wamesema wapo tayari kuchangia endapo utaratibu wa Uchangiaji utawekwa wazi.