Wazazi Chanzo Cha Ukatili Kwa Watoto,Malinyi na Ifakara
25 June 2021, 6:06 am
Na: Katalina Liombechi.
Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Mathayo Masele ameyasema hayo wakati akizungumza na Radio Pambazuko kwa Njia ya Simu ilipotaka kujua ukubwa wa changamoto ya vitendo hivyo kwa watoto katika Wilaya hiyo.
Masele amekiri kuwepo kwa changamoto hizo ambazo kwa namna moja au nyingine wamekuwa wakikabilina nazo kwa kuwachukulia hatua za kisheria watu wanaohusika na vitendo hivyo pamoja na kutoa Elimu kwa jamii kuhusu suala la Ulinzi na Usalama wa Mtoto.
Mlezi wa Kituo cha Watoto yatima cha EBENEZA kilichopo katika Halmashauri ya Mji wa Ifakara Mama Tecla amesema changamoto zinazowakuta watoto wengi zinasababishwa na wazazi wenyewe huku jamii ikipuuza pale inapoona watoto wanapata mateso.
Baadhi ya Watoto kutoka katika Kituo cha EBENEZA wameelezea namna walivyokutana na madhira mbalimbali ambayo yamewakuta mara baada ya kufiwa na wazazi kutengana.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Kilombero kupitia chama cha Mapinduzi Ngariri Ngariri amesema wamekuwa wakifanya ziara za kusikiliza changamoto mbalimbali za watoto na kutoa Maelekezo kwa Serikali kushughulikia changamoto hizo.