Triple A FM

Mtoto kwanza mengine yafuate

7 October 2026, 10:30 pm

Picha unde ikimuonesha mzazi anayemfundisha mtoto wake maadili mema

Na Fedrick Mbaruk

Wananchi Mkoani Arusha wamewaomba viongozi wa serikali za mitaa kuongeza elimu kwa jamii kuhusu namna ya kukabiliana na vitendo vya ukatili dhidi ya watoto

Miongoni mwa vitendo vilivyotajwa kukithiri kwa wazazi hao ni Pamoja na ubakaji na ulawiti, huku wakisisitiza umuhimu wa wazazi na walezi kuwa karibu na watoto wao

Maoni hayo wameyatoa katika mahojiano waliyofanyiwa na mwandishi wetu ambapo wameeleza kuwa baadhi ya wazazi wamekuwa wakitumia muda mwingi kutafuta mahitaji ya familia na kufanya shughuli za kiuchumi, hali wanayodai inaweza kupunguza muda wa kuwafuatilia watoto na kujua changamoto wanazopitia.

Wananchi wakitoa maoni

Wameeleza kuwa jamii inapaswa kurejesha utamaduni wa ujirani mwema na malezi ya pamoja, kwa kuwa watoto mara nyingi hukutana na watu mbalimbali katika mazingira yao, hivyo usalama wao unahitaji ushirikiano wa jamii nzima.

Wananchi wakitoa maoni

Pia wamewataka wazazi na walezi kuwa na mawasiliano ya karibu na watoto wao ili wawe huru kuwaelezea changamoto wanazokutana nazo bila hofu.

Wananchi wakitoa maoni