Triple A FM

Picha nzima mauaji ya Rebecca wa BnB

9 October 2026, 9:19 am

Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha SACP Justine Masejo

“ila tulimkuta amelala, labda kama walifanya laikini sio hapa na sijui kama ni hapa au ni wapi ni kama vile walimvunja shingo maana ime….”

Na Joel Headman

Baada ya mauaji ya muhudumu katika nyumba ya wageni (BnB) mkoni Arusha hatimaye Jeshi la polisi mkoani hapa limethibitisha kushikiliwa kwa mtu mmoja

Kupitia taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha SACP Justine Masejo imeeleza kuwa binti huyo aliyefahamika kwa majina ya Rebecca Naffi miaka 22, alikutwa amefariki usiku wa Oktoba 08, 2026 ndani ya nyumba aliyokuwa anaishi, iliyopo kata ya Ambureni Wilayani Arumeru

Kamanda Masejo ameeleza kuwa uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea na kuwarai wananchi kutoa taarifa zitakazosaidia kupatikana kwa wahusika wa tukio hilo

Akielezea tukio hilo mwenyekiti wa mtaa Evarest Lazaro amelitaja kuwa la kustaajabisha na la ukatili lisilovumilika akihitaji hatua mathubuti ili kukomesha matukio ya iana hiyo

Mwenyekiti wa mtaa Evarest Lazaro

Kwa upande wake Sandito Kaaya ambaye ni jirani wa nyumba hiyo amewasihi wananchi hasa mkoani Arusha kufanya maombi ili kusaidia kupunguza au kumaliza kabisa matukio ya aina hiyo

Sandito Kaaya jirani

Hata hivyo baada ya kuwasili eneo la tukio, Mkuu mpya wa wilaya ya Arumeru Neema Lugangira amelitaka jeshi la Polisi kuharakisha uchunguzi na kuwabaini wahusika wa tukio hilo

Mkuu wa wilaya ya Arumeru Neema Lugangira