Triple A FM
Triple A FM
19 October 2026, 9:57 am

Fedrick Mbaruku na Furahini Sella
Baada ya Serikali kupitia mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) kuja na uamuzi wa kusitisha matumizi ya vocha za kukwangua wakazi Mkoani Arusha, wametoa maoni na mitazamo yao juu ya uamuzi huo
Miongoni mwa wananchi hao wameeleza kuwa hatua hio inaweza kurahisisha upatikanaji wa huduma za mawasiliano na kuendana na maendeleo ya teknolojia.
Wametoa maoni hay leo wakati wakizungumza na Triple A FM na kueleza kuwa utaratibu huo unaweza kumsaidia mtumiaji kununua muda wa maongezi au kifurushi moja kwa moja kupitia simu yake, bila kulazimika kutafuta vocha ya kukwangua.
Hata hivyo, wamesisitiza umuhimu wa kuhakikisha kuwa mabadiliko hayo yanafanyika kwa kuzingatia mahitaji na mazingira ya watumiaji mbalimbali.
Hata hivyo wameeleza kuwa pamoja na faida za mfumo huo, kuna haja ya kuzingatia wananchi ambao hawana simu janja, ujuzi wa kutosha wa teknolojia au upatikanaji wa uhakika wa huduma za mitandao, hususan katika maeneo ya vijijini na kutaka Kundi hilo lisiachwe nyuma
Kwa mujibu wa TCRA Mikoa ya Arusha, Dar es salaam,Dodoma, Mwanza na Mbeya itakuwa katika hatua za majaribio ya kusitisha matumizi ya kadi hizo kuanzia Januari Mosi, 2027 huku uhamasishaji wa wananchi ukiendelea