Triple A FM
Triple A FM
2 September 2026, 4:11 pm

Tunatafuta temporary measure huduma iweze kurejea…Atleast kwa leo tutapambana kwa sababu,,,,,,,
Na Fedrick Mbaruku
Baadhi ya wananchi wa mtaa wa National housing kata ya Ngarenaro jijini Arusha wamelalamika kukosa huduma ya maji kwa muda tangu kuanza kwa zoezi la upanuzi wa barabara inayoanzia kona Nairobi kuelekea Barabara kuu ya Arusha Namanga
Wakiwasilisha malalamiko yao kwa nyakati tofauti kupitia kipindi cha jambo Tanzania kinachoruka Jumatatu mpaka Ijumaa asubuhi, wameeleza kutatizika kwa shughuli mbalimbali za kimaendeleo kutokana na kukosa maji
Baada ya malalamiko hayo Triple A fm imeutafuta uongozi wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mkoa wa Arusha (AUWSA) ili kujua ni kwa namna gani tatizo hilo linapatiwa ufumbuzi wa kudumu
Kuitia afisa mahusiano wa AUWSA Bi.Mary Maleko ameeleza kuwa kero hio ipo katika hatua za utatuzi na kuwa huduma yam aji itaanza kurejea mara moja kuanzia leo
Maleko amesema mamlaka hio inashirikiana na wakandarasi ili kuhakikisha huduma hiyo haitatiziki tena hasa wakati huu ambapo ujenzi unaendelea.
Hata hivyo amewaasa wananchi ambao wanashiriki au kufanikisha zoezi la kuhujumu miundombinu ya AUWSA ikiwemo wizi wa mita za maji