Triple A FM

Wanahabari wanawake waweka rekodi Arusha

17 March 2024, 10:21 pm

Mwenyekiti wa Arusha Women in Media Jamila Omar

Na Joel Headman

Umoja wa kwanza wa wanawake wanahabari ngazi ya mkoa nchini umezinduliwa mkoani Arusha.

Umoja huo uliopewa jina la Arusha Women in Media umezinduliwa jijini Arusha Jumamosi Machi 16, 2024.

Akizungumza mwenyekiti wa umoja huo Jamila Omar amesema una lengo la kuwaleta pamoja wanawake wanahabari mkoani Arusha kujadili mambo tofauti ndani na nje ya tasnia ya habari ikiwemo kujikwamua kiuchumi.

Mwenyekiti wa Arusha Women in Media Jamila Omar akieleza namna umoja huo ulivyoanzishwa

Jamila amewashauri wanawake kutafuta fursa mbalimbali ili kujikwamua kiuchumi na kuepuka kutegemea chanzo kimoja cha mapato kinachotokana na tasnia ya habari.

Mwenyekiti wa Arusha Women in Media Jamila Omar Akifafanua fursa zitakazowanufaisha wanawake wanahabari