Triple A FM

Mdahalo kufanyika kata kinara kwa ukeketaji Arusha

2 February 2024, 2:27 pm

Afisa Maendeleo ya Jamii,Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Helena Materu.picha na Anthony Masai.

“Vtendo vya ukeketaji nchini vimepungua lakini vimeongezeka kwa mkoa wa Arusha ambao unaongoza nchini kwa vitendo hivyo”

Na. Anthony Masai.

Maadhimisho ya kitaifa ya siku ya kupinga vitendo vya ukeketaji nchini yanatarajia kufanyika katika kijiji cha Olchorvosi,kata ya Musa,halmashauri ya Arusha Mkoani Arusha,Februari 6 mwaka huu chini ya kauli mbiu isemayo SAUTI YANGU HATIMA YANGU WEKEZA KWA MANUSURA KUTOKOMEZA UKEKETAJI.

Afisa Maendeleo ya Jamii,Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Helena Materu,amesema maadhimisho hayo yametanguliwa na wiki ya kuelimisha Umma kuhusu madhara ya ukeketaji,aidha utafanyika mdahalo mkubwa katika kijiji cha Olchorvosi ambako kuna matukio mengi ya ukeketaji.

sauti ya rehema materu,afisa maendeleo.

Kwa upande wake mmoja wa wajumbe wa mpango wa taifa wa kutokomeza ukatili wa kijinsia MTAKUWA kata ya Kiutu,Halmashauri ya Arusha Bi.Theresia Silikwa ,amesema ni wakati wa jamii kuanza kuweka mikakati dhidi ya mbinu mpya za ukeketaji zilizoibuka katika jamii.

sauti ya theresia Silikwa.