Triple A FM

Wanachama TADIO wanufaika na mafunzo ya kusimamia mitandao

8 December 2023, 11:16 pm

Washiriki kutoka redio Orkonerei Simanjiro wakipakia habari mtandaoni

Mabadiliko ya teknolojia yanakua kwa kasi hivyo TADIO inalazimika kutoa mafunzo mara kwa mara ili kubabiliana na mabadiliko hayo

Na Joel Headman Arusha

Muunganiko wa redio jamii Tanzania TADIO umekamilisha mafunzo ya siku mbili kwa wadau wa redio wanachama wa muunganiko huo kwa kanda ya Kaskazini.

Akihitimisha mafunzo hayo yaliyoanza jana Disemba 07, 2023 kwenye hoteli ya Eland Jijini Arusha, Mhariri wa TADIO Hilali Ruhundwa amesema mafunzo hayo yamekuwa ya mafanikio na kwamba wanategemea mabadiliko makubwa kwenye kwenye redio husika hasa kwa upande wa mtandaoni.

Sauti ya Hilali Ruhundwa mhariri wa TADIO

Akizungumza bi.Upendo Yohana mtaalamu wa TEHAMA kutoka redio Fm Manyara ambayo ni mwanachama mpya wa TADIO, amesema mafunzo hayo yatasaidia redio wanachama kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya Kiteknolojia ambayo yanakua kwa kasi.

Sauti ya Upendo Yohana mtaalamu wa TEHAMA

Kwa upande wake Gasper Joseph mwandishi wa habari kutoka redio Boma Hai FM mkoani Kilimanjaro, ameishukuru TADIO kwa mafunzo hayo na kuyataja kuwa ya mfano na yenye manufaa.

Sauti ya Gasper Joseph mwandishi wa habari
Waandishi wa habari wakipata mafunzo kwa vitendo

Muunganiko wa redio jamii Tanzania TADIO una jumla ya wanachama watano kwa kanda ya Kaskazini na umekuwa na utaratibu wa kukutana nao kutoa mafunzo tofauti tofauti ili kuwajengea uwezo.