Triple A FM

DSW yakutanisha vijana kujadili afya ya uzazi, ukatili wa kijinsia

10 April 2024, 7:36 pm

Winnie Muine, Meneja miradi wa shirika la DSW. Picha na Anthony Masai

“Vijana vinara wa vyuo vikuu na walio nje ya shule wamekuwa msaada mkubwa kufikisha elimu kwa vijana wengine nchini”

Na Anthony Masai

Shirika lisilo la kiserikali la DSW lenye makao yake makuu Tengeru wilaya ya Arumeru mkoani Arusha, katika kutekeleza mradi wake wa SAFA unaowezesha vijana katika maeneo ya elimu ya afya ya uzazi, mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia, ujasiriamali na ajira; limewakutanisha vijana 1500 kuwajengea uwezo katika maeneo hayo ya mradi.

Meneja miradi wa DSW Winnie Muine amesema vijana hao wanatoka mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Mbeya, Songwe na Manyara ambako mradi wa SAFA unatekelezwa ambapo vijana hao ni vinara ambao wanatarajia kuifikia jamii ya vijana wengi zaidi na kuwaelimisha waliyofundishwa.

Sauti ya Winnie Muine

Mkufunzi wa kitaifa wa masuala ya elimu ya afya ya uzazi kwa vijana na ukatili wa kijinsia Dkt. Erasi Nyari amesema tafiti zinaonesha kwamba bado idadi ya vijana wanaotumia njia za uzazi wa mpango iko chini nchini.

Sauti ya Dkt. Erasi Nyari

Kwa upande wake mmoja wa wanafunzi wa vyuo vikuu vinara katika uelimisha vijana Agusta Mapunda wa chuo kikuu cha Dar es Salaam Ndaki ya Afya na Sayansi shirikishi Mbeya amesema madawati ya jinsia vyuoni yamesaidia kupunguza adha kwa wanafunzi hasa ya kutakiwa kujihusisha kimapenzi na wakufunzi wao ili kufaulu masomo.

Sauti ya Agusta Mapunda