Triple A FM

Mifumo ya mahakama iliyoboreshwa yapunguza idadi ya mahabusu gereza kuu la Arusha

1 February 2024, 9:14 pm

Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela(mwenye suti) aliyekuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya siku ya sheria nchini,mkoa wa Arusha;katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali.picha na Anthony Masai.

“Wahalifu walipo gereza la Kisongo ni 704,asilimia 70 ni wafungwa na 30 ni mahabusu,tofauti na miaka ya nyuma ambapo ilikuwa kinyume chake”

Na. Anthony Masai.

Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu kanda ya Arusha Jaji Joackim Tinganga,amesema mabadiliko makubwa yaliyofanyika kwenye mifumo ya mahakama na vyombo vingine vya ufuatiliaji na utoaji haki nchini,yamefanikisha kupunguza msongamano wa mahabusu katika gereza kuu la Arusha-Kisongo kwani mashauri yanasikilizwa na kuamuliwa kwa wakati.

Amesema hayo hatika maadhimisho ya kilele cha wiki ya sheria nchini ,ambapo kwa Arusha yamefanyika katika viwanja vya mahakama jumuishi jijini hapa.

sauti ya jaji mfawidhi Joackim Tinganga

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela,amepongeza Mahakama kwa maboresho hayo kwani yanaleta mabadiliko katika michakato ya utoaji haki.

sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela.

Aidha chama cha mawakili Tanganyika TLS kupitia kwa Mwenyekiti wake kanda ya Arusha Bwana George Njooka,kimelikumbusha jeshi la polisi na vyombo vingine vya haki,kutambua uwakilishi wa watuhumiwa wanapoamua kuwatumia mawakili katika kutafuta haki zao.

sauti ya mwenyekiti wa TLS Arusha George Njooka.