Triple A FM

Arusha City yafungashiwa virago ASFC

16 December 2023, 10:25 pm

Mchezji wa Arusha City akiwania mpira na nahodha wa Singida FG Gadiel Michael picha na Joel Headman

Niwashukuru sana vijana wangu wameonyesha kiwango kizuri dhidi ya Singida maana wao wametuzidi vitu vingi

Joel Headman. Arusha

Unaweza kusema ni mkono wa bye bye ulioikuta timu ya mpira wa miguu ya Arusha City baada ya kuondoshwa kwenye michuano ya shirikisho nchini maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC)

Arusha City ambayo inashiriki ligi daraja la 3 mkoani Arusha iliangushiwa kipigo cha bao 3-0 kutoka kwa timu ya Singida Fountaion Gate inayoshiriki ligi kuu nchini

Mchezo huo uliopigwa kwenye uwanja wa Black Rhino Karatu Desemba15 ulianza kwa kasi na kuonekana Singida wakimiliki mchezo kwenye kipindi cha kwanza na kupata magoli mawili ya dakika ya 9 na 27 yakifungwa na wachezaji Yusuf Kagoma na mshambuliaji Elvis Rupia raia wa Kenya.

Hata hivyo hali iliwabadilikia Singida kunako dakika 45 za kipindi cha pili baada ya mabadiliko yaliyofanywa na mwalimu wa Arusha City Mahsin Bawaziri kuonesha soka safi na kuanzisha mashambulizi kadhaa ya kushtukiza ambayo hayakuzaa matunda.

Mwalimu Bawaziri akizungumza na Triple A fm uwanjani hapo amesema amefurahishwa na namna vijana wake walivyojituma licha ya kutoshinda mchezo wameonyesha vipaji walivyonavyo.

Mahsin Bawaziri kocha wa Arusha City

Kwa upande wake afisa habari wa Klabu ya Singida Hussein Masanza amewapongeza Arusha City na kusema wamecheza mchezo mzuri na kuwapa kazi ya ziada.

Hussein Masanza Afisa habari wa Singida FG