Triple A FM

Ndege kuruka saa 24 Arusha

7 December 2023, 1:43 pm

uwanja wa ndege wa Arusha unaoongoza kwa kupokea ndege nyingi nchini Tanzania.Picha na Anthony Masai.

Uwanja wa ndege wa Arusha ni uwanja unaoongoza kwa kupokea ndege nyingi kuliko viwanja vyote nchini Tanzania lakini hautumiki kwa saa 24 kwa sababu ya kukosa taa.

Na.Anthony Masai

Serikali ipo katika hatua za mwisho za kuanza kuweka taa katika uwanja wa ndege wa Arusha ili uwanja huo uanze kutumika kwa kuruka na kutua ndege kwa saa 24.

Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa amesema hayo wakati akijibu hoja ya Mbunge wa Arusha Mjini Mrisho Gambo kuhusu kusuasua kwa hatua hiyo ya kuweka taa katika uwanja huo ambao ni wa kwanza nchini kwa kupokea wageni wengi.

Sauti ya Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa.

licha ya kuipongeza serikali kwa kuendelea kuwekeza kwenye miundombinu ya viwanja vya ndege, mbunge Mrisho Gambo alitaka maelezo kuhusu uboreshaji wa uwanja wa ndege wa Arusha.

INSERT:MRISHO GAMBO.

sauti ya Mbunge wa Arusha Mjini Mrisho Gambo.

Uwanja wa ndege wa Arusha tayari umeboreshwa eneo la kutua na kurukia ndege kwa kuongeza urefu wa eneo hilo.