Triple A FM
Triple A FM
6 June 2025, 10:58 pm

Na Joel Headman
Naibu waziri mkuu dk. Dotto Biteko leo amefungua maonyesho ya kimataifa ya utalii ya Karibu Kili Fair 2025 jijini arusha
Akizungumza mkuu wa mauzo kwa wateja wakubwa na serikali kutoka kampuni ya YAS Anatory Lelo ameeleza kuwa wamejiandaa vyema kuhudumia wateja won a wapya kwenye maonyesho hayo.
Pia amewatoa hofu washiriki wa kimataifa kuwa kutakuwa na huduma ya vifurushi maalum vitakavyowafanya kuwa hewani kwenye mtandao kwa muda wote.
Kwa mujibu wa waandaaji wa tukio hilo linalofanyika kwenye viwanja wa Magereza Arusha, zaidi ya wanunuzi na mawakala wa usafiri 500 kutoka mataifa mbalimbali duniani watashiriki kwenye maonyesho hayo