Triple A FM

Mtandao nyaraka feki wanaswa Arusha

29 May 2026, 10:17 am

Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Arusha, Zawadi Ngailo

Na Furahini Sela

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Mkoa wa Arusha imezuia ubadhirifu wa zaidi ya shilingi bilioni tatu uliokuwa ukihusishwa na jaribio la kuuza viwanja vitatu katika Kata ya Levolosi, jijini Arusha.

Viwanja hivyo vinadaiwa kuuzwa kwa siri na msimamizi wa mirathi bila ridhaa ya familia, kwa bei ya chini pamoja na kukwepa kulipa kodi ya serikali.

Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Arusha, Zawadi Ngailo, ametoa taarifa hiyo wakati akiwasilisha ripoti ya utendaji kazi wa taasisi kwa kipindi cha miezi mitatu.

Kwa upande wake, Kamishna Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Arusha, Frank Mizikuntwa, amesema walipokea malalamiko kutoka kwa familia iliyodai kuwepo kwa udanganyifu wa nyaraka za mikataba

Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Arusha, Zawadi Ngailo