Triple A FM
Triple A FM
18 May 2026, 5:56 pm

“Tulifanikiwa kukamata watuhumiwa 19 wakiwa na mirungi kilo 90 na watuhumiwa 12….”
Na Joel Headman
Jeshi la polisi mkoani Arusha limesema katika kipindi cha Aprili 18, 2026 hadi sasa, watuhumiwa 176 wamehukumiwa vifungo mbalimbali vya makosa ya jinai ikiwemo ulawiti, ubakaji, wizi, dawa za kulevya, pamoja na kupatikana na nyara za serikali baada ya kufikishwa Mahakamani
Akitoa taarifa hiyo leo Mei 18, 2026 Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha, SACP Justine Masejo amesema kati ya waliohukumiwa kwa makosa makubwa, mtuhumiwa 01 alihukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa kosa la mauaji huku mtuhumiwa 01 akihukumiwa kifungo cha maisha gerezani kwa kosa la kulawiti
Aidha, amebainisha kuwa kupitia operesheni dhidi ya dawa za kulevya, walifanikiwa kukamata watuhumiwa 19 wakiwa na Mirungi Kilogramu 90 na watuhumiwa 12 wakiwa na bangi misokoto 177